MPANGO AHITIMISHA MBIO ZA MWENGE MBEYA.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kita kwa mwaka huu Ismail Ali Ussi, amekabidhi Mwenge huku akisisitiza umuhimu wa usimamizi thabiti wa miradi mbalimbali iliyotembelewa na Mwenge huo.


Katika hotuba yake wakati wa kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Mbeya leo Oktoba 14,2025, Ussi amebainisha kuwa wakati wa mbio hizo, Mwenge umeshuhudia akinamama wakipata dawa na matibabu kwa wakati, huku huduma katika hospitali mbalimbali zikiwa zimeboreshwa, na kuwepo  usafiri wa uhakika.


Aidha, ameongeza kuwa wananchi wanaishukuru Serikali kwa kuwapelekea huduma ya maji safi na salama, huku wakiomba huduma hiyo iendelee kusambazwa katika maeneo ambayo bado hijakidhi.


Vilevile Ussi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuzielekeza halmashauri zote nchini kutenga fedha kwa ajili ya mikopo ya vijana, wanawake, na makundi maalum, ili waweze kukamilisha miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa.

Comments

Popular Posts