SERIKALI YATANGAZA AJIRA MPYA 41,500
Serikali imetangaza nafasi za ajira 41,500 za kada mbalimbali, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2025/26 na kuwataka Watanzania wenye sifa kuchangamkia fursa hiyo.
Ajira hizo ni katika kada za elimu nafasi 12,176, sekta ya afya ngazi ya serikali za mitaa (10,280), kilimo (470), mifugo (312), uvuvi (47), ulinzi inayohusisha Jeshi la Polisi, magereza, zimamoto na uhamiaji (7000) pamoja na kada nyingine.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumshi wa Umma na Utawala Bora, Juma Mkomi amesema hayo leo Oktoba 11, 2025 jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ajira zilizotengwa na serikali kwa mwaka 2025/26.
“Ninaelekeza Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kuanza mchakato wa kujaza nafasi hizi za mwaka 2025/26 pamoja na kukamilisha mchakato wa nafasi zote za mwaka 2024/25.
“Ili kuhakikisha Sekretarieti ya Ajira inatekeleza jukumu hili ipasavyo, waajiri wote wanaelekezwa kutoa ushirikiano,” amesema
Ameongeza kuwa ili kupunguza gharama za usaili, Sekretarieti ya Ajira


Comments
Post a Comment