WANAO TUMIA FEDHA ZA UMA KUCHELEWESHA MIRADI YA SERIKALI WATAWAJIBISHWA.
Waziri wa Madini Antony Mavunde ameelekeza kuchukuliwa kwa hatua za haraka kwa watu wanaotumia pesa za umma na kuchelewesha miradi mbalimbali ya maendeleo
Ameongea na wananchi wa kijiji cha ushirika katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita wakati alipopita kuweka jiwe la msingi katika hospital ya ushirika ambayo ilikuwa imekwama kuendelea kutokana na baadhi ya watu kutumia vibaya pesa za mradi huo.
Serikali ilitenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho cha afya ambazo zilishindwa kusimamiwa vizuri na kushindwa kumaliza kituo hicho cha afya hivyo kuilazimu serikali kuongeza milion 60 nyingine ambazo bado hazijaanza kufanyiwa kazi.
Zaidi ya watu elfu 35000 wanatarajiwa kupata huduma katika kituo hicho Ambao ni muunganiko wa kata tatu.
Mavunde amemuelekeza mhandisi ambaye ni mgeni katika mradi huo kuhakikisha ndani ya wiki moja tenda inatangazwa ili kuingiza kwenye mfumo ili kuweza kumalizia pesa zilizobaki na kumalizia mradi huo.
"Kuna baadhi ya maeneo yana kasoro hasa katika milango nimeelekeza yarudiwe na kuweka milango bora" alisema Mavunde.
Mkuu wa mkoa wa Geita Martin Shigela alisema kuwa wahusika wote waliohusika katika kukwamisha mradi huo wameanza kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kimahakama.
Wananchi wa kijiji cha ushirika wameishuru serikali ya awamu ya nne kwa kuwasogezea huduma za afya karibu kwani hapo nyuma kina mama walijifungulia njiani.
#NangaMedia



Comments
Post a Comment