RC. CHALAMILA : NITAFANYA ZIARA ZA USIKU WA MANANE.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametangaza kufanya ziara ya usiku wa Manane kwa siku nne mfululizo itakayoanza Oktoba 22-25 itakayokuwa inaanza saa2 usiku hadi saa 12 asubuhi kwa lengo la kuangalia mienendo ya utoaji wa huduma muhimu za jamii.
Chalamila amesema kwenye ziara hiyo atakagua mwenendo wa utoaji wa huduma za afya kwenye Hospitali za mkoa wa Dar eś Salaam, lakini pia atakagua mitaa ambayo inasemwa ina Taa lakini Taa hizo hazifanyi kazi na atatoa maagizo ya muda gani Taa hizo zinatakiwa ziwe zimewaka kwenye maeneo yote ya mkoa ambayo yana nguzo za Taa lakini haziwaki.
Aidha RC Chalamila amesema atakagua mradi wa barabara za mwendokasi kutoka Moroco kwenda Tegeta, Mwenge kwenda Ubungo lakini pia atakagua sehemu zinazofanya biashara masaa24 ili kuona ni namna gani maboresho yanahitajika kabla ya kufungua soko la Kariakoo litakalokuwa linafanya kazi saa24, na miongoni mwa maeneo yatakayotembelewa ni Kariakoo, Manzese, Bunju, Gongo la Mboto na Mwananyamala ili kujionea maeneo gani yanahitaji maboresho.
Sehemu Nyingine itakayo guswa na ziara hiyo ni shule za Mabweni kuona mwenendo wa maadili, tabia na malezi ya wanafunzi.
Ofisi za Kamishna wa Ardhi mkoa wa Dar es Salaam zitakuwa wazi kwa siku hizo zote ili watu walioshindwa kupata huduma mchana waweze kupata huduma hiyo nyakati za usiku.
“Tutaangalia mwenendo wa usafi na uzoaji wa takataka hasa katika nyakati za usiku kwenye eneo la kuanzia Coco beach kuelekea Masaki kupitia Bwalo la Polisi.” Rc Chalamila



Comments
Post a Comment