NDEMLA: MAWAKALA WANAZINGUA
NDEMLA: MAWAKALA WANAZINGUA !!
Kiungo fundi wa mpira anyekipiga Singida Big Stars, Said Hamis Ndemla anasema kinachowakwamisha wachezaji wazawa kutoka nje ni kukosa mawakala wa kutengeneza dili zao, hivyo wanajikuta wakikwama kutimiza ndoto zao.
.
“Nimewahi kwenda kufanya majaribio Sweden klabu ya AFC Eskilstuna ya mjini Eskilstuna, nilifaulu lakini yapo mambo yaliyofanya nisicheze timu hiyo, makocha waliokuwa wananiangalia mazoezini na wachezaji walisema nina kipaji kikubwa,” anasema na kuishia hapo na kushindwa kueleza yote aliyopitia huko;
“Si kila kitu mchezaji anaweza akazungumza. Kuna wakati naona mengi kwenye mitandao ya kijamii kuona wazawa hatupambani, ila sio kila kitu kinachoandikwa unatakiwa kukijibu, mengine unayaacha yaende tu, binafsi nikipata wakala mzuri nipo tayari kwenda nje.”
Nanga Media tz 🇹🇿🇹🇿🇹🇿




Comments
Post a Comment