RASMI MH.MAKONDA AKABIDHI OFISI KWA RC KUNENGE, ASEMA MAKUBWA
Aliekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* leo Agost 03 *amekabidhi rasmi ofisi* kwa Mkuu wa Mkoa huo *Mhe. Aboubakar Kunenge* ambapo amesema ataendelea *kusimama kidete kumlinda* na kumuunga mkono *Rais Dkt. John Magufuli* kwenye kila jambo kwakuwa ndio *"Role Model"* wake.

*Mhe. Makonda* amesema anajisikia *amani na furaha* kwa kumaliza safari yake ya *utumishi katika Mkoa wa Dar es salaam* akiwa *ameacha alama kubwa* kwa jamii, taasisi na *kugusa maisha ya mmoja mmoja.*
Aidha *Mhe. Makonda* amesema kwa sasa ataendelea kuwa *mshauri mambo mbalimbali yenye kuleta maendeleo kwa mkoa na Taifa kwa ujumla* kwakuwa *yapo mengi aliyojifunza* katika safari yake ya utumishi.

Pamoja na hayo *Mhe. Makonda* amesema kwa sasa analo jukumu la kuendelea kuhakikisha *Rais Dkt. John Magufuli* anapata *ushindi wa kishindo* katika Uchaguzi Mkuu ikiwa ni pamoja na *Wabunge na Madiwani wa Chama cha Mapinduzi CCM.*
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Aboubakar Kunenge* amesema ataendelea *kupokea ushauri* mbalimbali anaopatiwa na *Mhe. Makonda* kwakuwa amekuwa *mwalimu na mshauri wake* katika mambo mbalimbali tokea walipoanza kufanya kazi pamoja.
Aidha *RC Kunenge* ameeleza kuwa wataendelea *kumuenzi na kumueshimu* kwa mchango mkubwa wa *mabadiliko ya kimaendeleo aliyofanya katika Mkoa huo.*



Comments
Post a Comment