Malawi kufanya Uchaguzi wa Rais kwa mara ya pili leo.


Watu nchini Malawi leo wanapiga kura ya kumchagua Rais kwa mara ya pili baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana kubatilishwa na Mahakama.

Mwezi wa Februari, Mahakama ya Katiba iliamuru uchaguzi huo ufanyike tena baada ya kutoa hukumu kwamba matokeo ya uchaguzi wa kwanza yalikuwa batili kutokana na ushahidi uliobainisha hitilafu kadhaa na udanganyifu katika hesabu za kura.

Mahakama iliufutilia mbali ushindi wa Rais Peter Mutharika aliyekuwa mamlakani, vituo zaidi ya 5000 vimefunguliwa Malawi kote kwa ajili Watu Millioni 6.8 wanaostahiki kupiga kura.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewataka viongozi wa kisiasa na wadau wengine wote wahakikishe kwamba uchaguzi unafanyika kwa njia ya haki na kwa amani
(via @dw_kiswahili )

Comments

Popular Posts