Waziri avifuta vyama 3,348 vya ushirika




Waziri wa Kilimo leo amevifuta Vyama vya Ushirika 3,348 ambavyo vingi ni hewa huku ikisema zoezi la kufuta Vyama hivyo litakua endelevu kwa Vyama visivyo fuata sheria Na. 6 ya Mwaka 2013.
.
.
.
Vyama ambavyo vimefutwa ni SACCOS 2,513, AMCOS 229, Mifugo 77, Vyama vya Walaji 27, Vyama vya Huduma 70, Vyama vya Ufugaji Nyuki 15, Vyama vya wenye nyumba 9, Vyama vya Madini 22, Vyama vya wenye Viwanda 79, Vyama vya Uvuvi 32, Vyama vya Umwagiliaji 31 na vingine 244.
.
.
.
Kabla ya kufutwa vyama hivyo, Vyama vya Ushirika vilikua 11,626 baada ya kufutwa vyama 3,348 vimebaki 8,611.
.
.
.
Waziri amewataka wanachama na wakulima kufunga akaunti benki ili Mkulima kujihakikishia malipo yake.ili kuondoa udanganyifu unaofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama malipo.
.
.
.
Akizungumzia mfumo wa ununuzi wa mazao Nchi nzima, Waziri Hasunga amesema njia pekee ya kumkomboa Mwananchi ni kupitia ushirika
"Wananchi wakiuza Kwa pamoja ni rahisi kupata bei nzuri, hata hivyo kumetokhivyoea malalamiko mengi katika baadhi ya mikoa kuwa Wananchi wananyanyasika sana na mfumo wa vyama vya ushirika na stakabadhi ghalani..
.
.
.
Sasa ili mfumo wa stakabadhi ghalani uweze kufanyika sawasawa, naagiza kuwepo kwa Chama cha Msingi (AMCOS) kilichosajiliwa katika kijiji husika, kuwepo kwa ghala lililosajiliwa na Bodi ya Leseni za Maghala, kuwepo kwa mfumo wa kufanya minada kwa njia ya ushirika na kuwepo kwa Wanunuzi wa kununua kwa minada," Amesema Waziri Hasunga.
.
.
.
Waziri Hasunga ameagiza kila kijiji kiwe na soko la awali ambalo Wananchi watauza mazao yao lakini pia kuwe na soko la upili ambalo Wananchi, Vyama vya Ushirika na Wafanyabiashara wa ndani wataruhusiwa kuuza mazao yao kwa Wafanyabiashara wa nje.
.
.
.
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Vyama vya Ushirika nchini, Dkt. Titus Kamani ameishukuru Serikali
"Niipongeze sana Serikali imekua mara zote ikiwajali sana Wanachama wa Ushirika ambao wengi wao ni wanyonge na ndio maana tunaona mara kadhaa vyama hivi vinapoenda kinyume basi serikali kupitia Wizara ya Kilimo imekua ikichukua hatua kali ikiwemo kuvifutia usajili vyama vinavyoenda kinyume na uanzishwaji wake."

Comments

Popular Posts