MIL. 53 ZA SERIKALI KUOKOA WANANCHI SAME.



Serikali imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madaraja yaliyovunjika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Wilayani Same.

Akikagua maeneo hayo DC Same alisema; serikali ya CCM inayoongozwa na Mh. Dr. John Pombe Magufuli kwa kujali wananchi wake; imetoa fedha hizo ambazo hazikuwepo kwenye bajeti ili kujenga madaraja mawili

1. Daraja linalounganisha kata ya Kisiwani na Msindo lililopewa Tshs. 17M

2. Daraja linalounganisha kata ya Vumari na Same mjini ambapo Tshs 36M zimetolewa.

👉🏽" *Serikali imetoa fedha hizi ili kuwaondolea wananchi adha ya usafiri. Hivyo wakandarasi mliopewa kazi hakikisheni mnaifanya kwa ubora na kwa wakati. Ili dhamira njema ya Mh. Rais iweze kufikiwa* ". Alisema DC Same.

Alimshukuru Rais kwa fedha hizo na kuwataka wananchi kumuunga mkono kwa kutumia madaraja hayo kuboresha uchumi.

Pia aliwakumbusha wananchi kuendelea kujikinga na corona kwa kuzingatia maelekezo ya serikali.
.
.
#MakiniUpdate 

Comments

Popular Posts