Wanao rusha taarifa za uongo kuhusu CORONA watachukuliwa hatua za kisheria
DKT ABBASI AZUNGUMZIA WANAO RUSHA TAARIFA ZA UONGO MITANDAONI KUHUSU CORONA ZINAZO ZUA TAHARUKI KWA WANANCHI*

“Mpaka sasa taarifa za kuzusha kuhusu COVID-19 zipo katika mitandao ya kijamii, niwakumbushe tu Sheria zetu zipo na zinafanya kazi, watanzania lazima tuhakikishe tunaisaidia jamii kuondokana na huu ugonjwa, tuache kusababisha taharuki” amesema Dkt. Hassan Abbasi
“Wakati tunaeleza ukweli kuhusu ugonjwa huu wa COVID-19 pia waandishi wa habari tueleze tatizo lilivyo na namna ya kuondokana na tatizo, Nchi yetu katika mapambano ya ugonjwa huu wa COVID-19 tumechukua hatua na tutaendelea kuchukua hatua kukabiliana nao” amesema Dkt. Hassan Abbasi
“Lazima vyombo vya habari vichukue tahadhari wakati huu tukiwa kwenye majukumu yetu ya kuhabarisha umma, Idara ya Habari-MAELEZO tumetoa muongozo kwa waandishi wa habari wa namna ya kutekeleza majukumu yao, tuutumie” amesema Dkt Hassan Abbasi
“Tumeanza kutafakari namna tutakavyoendesha mikutano na waandishi wa habari, ikiwamo kutoa ‘Press Releases’, kurusha moja kwa moja na kusambaza ‘cleanfeed’ au kurekodi na kusambaza taarifa hiyo kwa waandishi wa habari,lengo ni kuepuka mikusanyiko” amesema Dkt.Hassan Abbasi


Comments
Post a Comment