UDHIBITI WA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA CORONA (COVID-19) WILAYANI SERENGETI.

#Sengerema
Mkuu wa wilaya ya Serengeti Mh.Nurdin Babu pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama ya wilaya na Mganga mkuu wa wilaya Bi.Emiliana Donald wanaendelea kutembelea kata, vijiji na vitongoji ili kuwaelimisha wananchi namna bora ya kujikinga na maambukizi ya corona.

Ziara hiyo ya kuwaelimisha wananchi imefanyika katika vijiji vifuatavyo:-
1.Ketarungu na Nyansurura kata ya Nyansurura.
2.Borenga kata ya Kisaka.
3.Nyamihuru kata ya Busawe.
4.Majimoto kata ya Majimoto.
5.Nyagasense kata ya Kenyamoto
6.Kibeyo kata ya Kisangura.
7.Kitunguruma kata ya Mbalibali
8.Nyamakendo na Machochwe kata ya Machochwe


Mh.Babu amewasisitisha wananchi hususani wafanyabiashara kuweka vitakasa mikono na sabuni kila duka na sehemu ambayo kuna mikusanyiko ya watu wengi .

Babu amewaomba sana kufuata taratibu zote zinazofundishwa na kutolewa na wizara ya afya ili kuweza kuepukana na janga hilo la ugonjwa wa corona (COVI-19), Corona aina tiba ila hutibiwa kutokana na dalili anazoonyesha mgonjwa.


Aidha amewasihi wananchi kuwa Serengeti ni miongoni mwa wilaya iliyopo jirani na nchi jirani ya Kenya, Kenya maambukizi ya Corona yanaendelea kuongezeka hivyo basi kuna baadhi ya wakenya wameanza kukimbilia kwa ndugu zao waliopo Serengeti kwa ajili ya kutoroka, anawaomba wananchi kuwa wakiona mgeni yeyote watoe taarifa kwa viongozi wa serikali ili kuweza kumchukua na kumuweka karantini kwa siku kumi na nne kama hana maambukizi ya virusi vya corona anaachiwa.

Akitoa elimu hiyo mbele ya wananchi Babu amepiga marufuku mikusanyiko ya harusi bali amewaomba kama kuna harusi wawe wanaenda walengwa tu idadi ya watu wasiozidi saba.
Mganga mkuu wa wilaya Bi.Emiliana amewaomba sana wananchi kuzingatia masharti yanayotolewa na wizara ya afya na kama kuna mgonjwa anahisiwa awahi kituo cha afya kilichopo karibu nae kwa msaada zaidi au kupiga simu bure 199 .

Pia Mkuu wa polisi wilaya (OCD) Ndg.Mathew Mgema amesisitisha wananchi kufuata masharti hayo na kuomba wazazi wakae na watoto wao nyumbani wasiende kuzurura mitaani
.
Ndg Mgema amewaomba katika kipindi hiki cha Pasaka wananchi waepukane na mikusanyiko isiyo ya lazima ili tuweze kupambana na janga hilo la corona aidha amewaonya wanaokeketa wasichana wakome mara moja maana atasukuma ndani na sheria itachukua mkondo wake kwa sababu ya unyanyazaji wa kijinsia.
Wananchi nao wamemshukuru mkuu wa wilaya pamoja na timu yake kwa ajili ya kuwapelekea elimu na kumhaidi watatekeleza.


Ziara ya kuwaelimisha wananchi namna ya kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa corona bado unaendelea lengo kuu ni kuhakikisha Serengeti kuwa salama, Babu anawaomba sana wananchi waendelea kumuomba Mungu (Allah) ili atuzaidie janga hilo liweze kupotea kabisa kama Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli aliposema hawezi kufunga makanisa wala misikiti corona ni pepo tulikemea kwa kumuomba Mungu.

Comments

Popular Posts