Tanzania kufanya maombi ya kitaifa
#MakiniUpdate
"Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na viongozi wa madhehebu ya dini nchini, imeandaa maombi maalum kitaifa,ili kuiombea nchi dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayotokana na virusi vya Corona.
Maombi hayo yatakayoongozwa na viongozi wakuu wa madhehebu ya dini nchini, yatafanyika Jumatano Aprili 22, 2020 viwanja vya Karimjee Jijini Dar Es Salaam, kuanzia Saa 3.00 Asubuhi. Mgeni rasmi atakuwa Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania.
Viongozi wachache watahudhuria maombi haya kuwakilisha wananchi ikiwa ni kuchukua tahadhari ya maambukizi, hivyo wananchi mnasisitizwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona na kufuatilia maombi mkiwa maeneo yenu kupitia vyombo vya habari" - Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.
#MaombiYaKitaifa



Comments
Post a Comment