RIPOTI YA BENKI YA DUNIA, KUPOROMOKA KWA UCHUMI AFRIKA


Ripoti ya Benki ya Dunia kuhusu hali ya kiuchumi Afrika imesema uchumi wa Afrika utashuka kwa 2.1% na kufikia 5.1% kutoka kiwango cha ukuaji cha mwaka jana cha 2.4%, hii ni kufuatia kuvurugwa kwa shughuli nyingi za kibiashara na kiuchumi kutokana na corona.

Ripoti hiyo imesema mlipuko hwa virusi vya corona utazigharimu Nchi za ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara Barani Afrika Dola Billion 37 hadi dola Billion 79 ambayo ni hasara itakayoonekana mwaka huu, huu ni mporomoko wa kwanza katika kipindi cha miaka 25.




Afrika ina takribani visa 10,956 vya Watu waliothibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona, vifo 562 na waliopona wakiwa ni 1,149 kwa mujibu wa takwimu za Shirika la habari la Reuters kwa kuzingatia taarifa zilizokwishatolewa na Serikali na data za shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).
( via @dw_kiswahili )

Comments

Popular Posts