#PWANI :- *"Msichukulie Mzaa Ugonjwa wa Corona"*

#MakiniUpdate


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi. Evarist Ndikilo leo tarehe 20 Aprili 2020 amewahimiza Wananachi  wa Mkoa huo kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona.

amewahimiza Wananchi wote wa Mkoa huo Kuvaa Barakoa wanapokwenda katika Ofisi mbali mbali za Umma na Binafsi ikiwemo Ofisi yake, kwenye Daladala, Bodaboda na maeneo ya Biashara ikiwemo Sokoni.

Aidha, amewahimiza kunawa kila mara kwa Maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono,kukaa umbali wa mita moja na mwezio, na kutoa Taarifa pale wanapohisi kuwa wanadalili za Maambukizi ya Virusi vya Corona.

Pia ameongezea kuwa tayari Mkoa una Mgonjwa mmoja na  Mkoa Pwani upo karibu na Dar es salaam penye wagonjwa wengi amewataka Wananchi  kujilinda  kwa kuchukua tahadhari zote Muhimu.

Mhandisi Ndikilo ameyasema hayo katika ziara fupi  Wilayani Kibaha (Sokoni, Stendi  na Maeneo ya  Biashara)  iliyolenga kukagua utekelezaji wa tahadhari zinazotolewa katika Kuthibiti maambukizi ya Virusi vya corona.

Comments

Popular Posts