MDEE ATEMA CHECHE BUNGENI KUHUSU CORONA
#HABARI
#VirusiVyaCorona TANZANIA; Katika Mkutano wa 16 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, unaoendelea mjini Dodoma leo, mbunge wa Kawe Halima Mdee, ameomba ufafanuzi kutoka Spika wa Bunge Job ndugai kuhusu bunge kuitaka serikali kutoa taarifa kwa Bunge juu ya hali ya Virusi vya Corona nchini,ili bunge lijadili kwa kina na kuangalia mpango wa Serikali wa dharura ili kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.
"Mh Spika nilikuwa naomba kupata ufafanuzi kutoka kwako katika kipindi hiki cha Bunge, nilidhani ni busara kwa Serikali kuja kutoa taarifa kwa Bunge juu ya hali ya Corona nchini, tulijadili kwa kina na tuangalie mpango wa Serikali wa dharura"
"Nadhani kama nchi kuna hatua kubwa zinapaswa kuchukuliwa na haiwezekani bila kupata 'proper report', tuulize maswali tujibiwe ili tuweze kuokoa wananchi, kama Marekani dunia ya kwanza inatapatapa, Italy na Spain pia, hili jambo ni kubwa" - Mbunge wa Kawe, Halima Mdee
(Picha/Maktaba)
#EpukaMikusanyiko
#JIHADHARI
#JikingeNaVirusiVyaCorona
#ChukuaTahadhari
#NawaMikono #MaraKwaMara
#CoronaNoma
#EpukaMikusanyiko
#JIHADHARI
#JikingeNaVirusiVyaCorona
#ChukuaTahadhari
#NawaMikono #MaraKwaMara
#CoronaNoma



Comments
Post a Comment