UJENZI WA NJIA ZA KUPITISHA UMEME RELI YA SGR DAR-MORO WAFIKIA ASILIMIA 87

#Utekelezaji
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Zena Saidi amesema kuwa Serikali itahakikisha umeme wa uhakika utapatikana kwa ajili ya kuendesha Treni ya Umeme na kazi imeanza ya kupitisha njia za umeme huo.
Akiongea wakati wa ziara ya Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara Mhandisi Zena amesema kuwa njia za kupitisha umeme kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro tayari imeshafikia asilimia 87.
Mhandisi Zena aliongeza kuwa nija za umeme kutoka Morogoro kwenda Ihumwa hadi Makutopora (Singida) kazi ipo katika hatua tofauti, ikiwemo kuingia katika majadiliano na nyingine tayari zabuni imeshatangazwa na mwezi huu wa tatu zitapokelewa.
Serikali ya Tanzania imekwishatumia takribani TZS trilioni 3 katika mradi huo wa TZS Trilioni 7 ambapo ujenzi wake, kwa sasa ni kipande cha kutoka Dar es Salaam- hadi Morogoro na Morogoro hadi Makutupora (Singida).

Comments

Popular Posts