Kalemani :- Natoa onyo la mwisho

#DODOMA  Kuna shida moja na hili ni onyo la mwisho. Nimepita barabarani. Nimekuta nguzo zimelala, sasa meneja wa Tanesco Kanda (ya kati) na mkoa (Dodoma) simamia maelekezo haya.

Nimetoa muda wa siku tatu nguzo zote zilizolazwa chini mkoa mzima wa Dodoma ziondolewe zikajengwe.

Nasema siku tatu kutoka leo nguzo ziondolewe, tofauti na hivyo mhandisi achia ngazi, mkandarasi utaandikiwa barua ya kufuta mkataba wako, nakueleza mapema, meneja lisimamie hili,

Na hili ni onyo kwa wakandarasi wote nchi nzima, ni marufuku kuanzia sasa nguzo kulazwa chini kwa muda mrefu, zikifika ndani ya siku tatu zikasimikwe na zikajengwe ili wananchi wakapate umeme.- Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani.


Comments

Popular Posts