MAWAZO YA BIASHARA NDOGO NDOGO, KUANZIA MTAJI WA ELFU 10-50.

#Darasa

1,DAGAA WA BUKOBA
Dagaa hawa wanapatikana masoko mengi, hawa wanakua hawana mchanga kabisa, wanauzwa kg moja elfu nane huwa inashuka had elfu tano, hawa unanunua vifuko unapack unauza mtaani kifuko buku
Kwenye kilo moja unaweza toa vifuko 15 sawa na elfu kumi na tano so elfu mbili vifuko elfu tano faida. Pia unaweza uza dagaa wa kigoma, zanzibar au mwanza waliokangwa

BIASHARA YA MATUNDA
Siku hzi watu wengi hasa maofisini wanapenda kula matunda andaa kwa usafi matunda yako hapa unaweza tumia elfu kumi na tano.
Unanunua matunda mchanganyiko, nunua vifungashio vile vya kuwekea matunda pack matunda yako ambapo yakiuzika vyema unaondoka na faida nusu kwa nusu

JUICE ZA MATUNDA,
Matunda ya elfu kumi waweza toa had lita kumi za juice ambapo lita moja ni sawa na glass tano au nne za juice so kwenye lita kumi upata grass 40 sawa na elfu ishirin ukitoa matunda,sukar na vigras unafaida elfu tano,
BIASHARA YA MKAA
Gunia la elfu 30 unaweza kutoa mafungu 45 ya mkaa sawa na elfu arobain na tano faida elfu kumi na tano

MOBILE GENGE,(GENGE LINALOTEMBEA)
Watu wengi sasa hiv mna smartphone tangaza unauza nyanya, vitunguu karoti, na mazagazaga mengine ya jikoni, ukipata order unaenda ilala soko la wakulima unajumua vya kutosha unapeleka faida hapa ni nusu kwa nusu, pia unaweza tembezea majirani zako kutegemeanana sehemu unayoishi,

BIASHARA YA BITES
Hapa nazungumzia crips sambusa chapati maandazi mihogo ya kukaanga, vitumbua karanga za mayai, ubuyu, korosho, visheti etc unaweza sambaza vitafunwa maofisini as package kwamba pack moja ina andaz sambusa chapati na kachori au ukauzia nyumbani moja ya vitafunwa hivyo, Bites as wel peleka kwenye maduka na supermaket faida yake huwa nusu kwa nusu

BIASHARA YA VINYWAJI BARIDI STEND ZA DALADALA
Unaweza uza hata kwenye ndoo kama huna deli, nunua mabarafu nunua vinywaji tafuta kijana au wewe mwenyewe uza stend za daladala inalipa saaana

BIASHARA YA UJI WA ULEZI, UJI WA MCHELE NA MAKANDE
Kodi toroli jaza chupa zako uji aina hzo tembeza kwenye magereji na sehem za bodaboda ..

BIASHARA YA SARAFU ZA KIDIJITALI(INA FAIDA KUBWA SANA)
Hapa unazungumzia Bitcoin,Etherium,Ripple,Stellar,EOS Na zingine zaidi ya aina 2000,Biashara hii kwa sasa ni ya Kidunia na inasemekana ndiyo Biashara yenye Faida na Mrejesho mkubwa wa haraka zaidi wa Mtaji wako,Hivyo Kikubwa sana hapa ni mtaji kuanzia Dola 100 awa na Tsh 230,000 hadi 25,000,000 za Kitanzania hapo utawza kujifunza na kuanza kupata faida kubwa sana..Kama ungependa kuijua Biashara Hii kwa kina Nitumie ujumbe Inbox nitakushauri Bure bila malipo..Karubu Endelea kuwa nami..

Kama umependa elimu hii Leo SHARE na wengine Tafadhali.

Comments

Popular Posts