Simba SC yaendelea kunoa makucha.

#MICHEZO

Mabigwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, SIMBA SC wameendelea kujinoa kuelekea michezo yao ya ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya MTIBWA FC tarehe 17.9.2019 uwanja wa uhuru Dar es Salaam, tarehe 22.9.2019 dhidi ya LIPULI FC uwanja wa uhuru Dar es Saalam.


Ikumbukwe kuwa mabingwa hao hawashiriki mashindano yeyote ya kimataifa, hii ni baada ya kutolewa katika hatua za awali za mashindano hayo.


Akinukuliwa kocha mkuu wa timu hiyo Aussems maarufu kama uchebe, amesema kuwa baada ya kutolewa katika mashindano ya kimataifa nguvu yao kubwa sasa wameiweka katika ligi kuu Tanzania Bara kwa kuhakikisha wanatetea vyema ubingwa wao.

Comments

Popular Posts