MAGONJWA YA KUKU NA TIBA

#MAKALA

YAFAHAMU MAGONJWA MBALIMBALI YANAYOSHAMBULIA KUKU. 

SEHEMU 1.

#KIDERI
  • Ugonjwa huu hutokea mara kwa mara na mara nyingi hushambulia kuku wadogo, na hata wakati mwengine kuku wakubwa.
  • huweza kusababisha vifo vingi (high flock mortality) na vifo hivi huwa kati ya asilimia 30 hadi 100 
#Dalili
  • Dalili muhimu za ugonjwa huu ni kama,
  1. Kukosa hamu ya kula, mfumo wa usagaji chakula kushindwa kufanya kazi inavyopaswa
  2. Kuharisha kijani
  3. Kupumua kwa shida
  4. Kuathirika kwa mfumo wa fahamu na kuku kupooza viungo.
#Tiba
  • Ugonjwa huu husababishwa na virusi na hivyo njia pekee ya kuepukana na ugonjwa huu ni kuwapa chanjo kuku wote bandani ikijumuisha vifaranga vya wiki mbili.
  • Pia kutumia viuadudu (Antibiotics) kama vile Oxyfarm 20% na Vitamini kuzuia magonjwa nyemelezi baada ya kuugua.

Comments

Popular Posts