GARDIEL AOMBA RADHI KWA WANAJANGWANI
Waraka wa Gardiel Michael kwa Young Africans SC
.
Wakati mwingine mtu unalazimika kufanya maamuzi yako peke yako kwa sababu anaewajibika na maisha yako mwisho wa siku ni mtu mwenyewe.
Mpira ndio kazi yangu ya kimaisha, maamuzi niliyoyafanya yalikuwa ni muhimu sasa kwa maslai yangu na familia yangu.
Nimuombe radhi aliekuwa meneja wangu Jemedari Saidi Kazumari kutokana na sintofahamu iliyotokea kwa kutomshirikisha nikiamini asingekubali nihame mtaa.
Nimelazimika kufanya maamuzi magumu kwa maslai mapana yangu mwenyewe na familia yangu.
Kikubwa ni kwamba Mpira ni familia moja, bado tuko kwenye familia, HAKUNA CHUKI, MAISHA YAENDELEE.
Niwashukuru wanaYanga wote kwa ushirikiano walioniptia, nilikuwa na furaha sana kwao. Pia niwashukuru viongozi wa Yanga chini ya mzee Msolla. Mimi ni mwanadamu, kiumbe dhaifu, Maana aliekamilika ni mola wetu pekee.
Nawaomba radhii sana.
Asante



Comments
Post a Comment