Walichokifanya Kiba na Samatta ni mfano wa kuigwa..
Repost from @officialchristz
HONGERENI SANA @officialalikiba NA @samagoal77
Hakika vijana wezety tuzidi kujifunza juu ya kutoa katika jamii inayotuzunguka hasa kwa wale watu wasio jiweza na wanaoishi katika mazingira magumu.
Alikiba na Samatta kupitia @samakibafoundation wametuonyesha kuwa wameamua kurudisha kwa jamii kile walichojaliwa na allha kwa njia hii nzuri kabisa ambayo naamini Njisi ambavyo miaka inavyozidi kwenda ndivyo unavyozidi kuongeza ladha ya Nifuate.
Tumejionea watu wakiwatunza hela watu wenye pesa ili hali kunawatoto wanao ishi katika maisha magumu na wadogo zetu wakiteseka kukaa chini madawati imekua shida ila wengine wanaonyesha jeuri hiyo ya fedha kwa wezao wenye pesa.
Unampomzawadia mwenye pesa sizani kama Mungu anakuongezea pale ulipotoa kwani unampa mtu mwenye nacho wakati kuna watu hawana hata senti tano na wanauhitaji mkubwa sana wa hizo fedha zako.
Ndugu zangu Vijana wezangu Mwenyezi Mungu akikujalia kupta pesa zitumie katika kuwekeza kwa watu wasiojiweza ili ujitengenezee Mbingu yako ilioyo bora sio kuishia kufanyia matanuzi na kubadili magari ya kifahari tu .
Ally kiba Na Samatta wanatukumbusha kuwa kule kijini kwetu tulikotoka kuna shisa turudi tukawasaidie vijana wadogo watimize ndoto zao kwani wengi wetu tukisha fanikiwa tunasahau hata nyuma tuliko toka na kuishia huku mjini kubali Mavazi na Magari ya bei kubwa
Ndio maana nimesema Asanten @officialalikiba na @samagoal77 kwa hili kupitia @samakibafoundation Mwenyezi Mungu awape Nguvu mzidi kujitoa katika Jamii inayowzunguka
Hongereni sana @hajismanara na @sudibrown213 kwa Kuweza kuhamasisha watu wakaja kusapoti hili




Comments
Post a Comment