TANZIA: Mchezaji Prison FC afariki dunia
"Tumepata msiba wa mchezaji wetu wa kikosi cha vijana U 20 Abdallah Mwinyimwaka ambaye alikuwa anasumbuliwa na Henia, alianza kuumwa mda sio mrefu tukawa tunamfanyia matibabu lakini dada yake akaomba akatibiwe Tanga na alipofika huko aliendelea na matibabu ikafikia hatua akafanyiwa upasuaji lakini akawa analalamika maumivu leo ikiwa ni siku mbili zimepita toka afanyiwe upasuaji huo tukapata taarifa kuwa amefariki, "
"Tunatarajia kuzika kesho na tumeshaanza taratibu kwa viongozi wa huku Mbeya kuelekea jijini Tanga kuungana na viongozi wengine wa Prisons pamoja na familia kwa ajili ya kumpumzisha mchezaji wetu, tumepoteza kijana ambaye naamini hapo baadaye angeweza kuiletea timu mafanikio wakubwa, kesho kwenye mechi yetu na lipuli U20 tutavaa vitambaa vyeusi kuomboleza, Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu pema peponi, " Ajabu Kifuke, Katibu Mkuu wa Tanzania Prisons.



Comments
Post a Comment