Kapombe: Niko fiti watanzania watarajie makubwa AFCON
SHOMARI KAPOMBE AREJEA, YUKO FITI
Beki wa kulia wa klabu ya Simba SC, Shomari Kapombe amewashukuru watanzania na wapenzi wa mpira wa miguu kwa kumuombea na sasa yupo vizuri kuanza kuitumikia klabu yake na timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'.
"Sijaonekana kwa muda mrefu na kila mtanzania anajua nilikuwa na majeraha ya muda mrefu ambayo niliyoweza kupata katika timu ya taifa",
"Hali yangu sasaivi naendelea vizuri na Mungu amenisaidia kuweza kuimalika siku baada ya siku naendelea kuimarika zaidi, Naweza kusema kwamba naheshimu maamuzi ya mwalimu (Amunike) kwa kuweza kunita na mimi siwezi kukata au kujiweka nyuma, napokea uwamuzi wake kwa kuweza kunita na mimi nitajiunga na timu ya Taifa" alisema Kapombe.
Beki huyo alipata majeraha mazoezini wakati akiwa na timu ya Taifa kabla kwenda kuwavaa Lesotho katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon.



Comments
Post a Comment