Zahera ashusha vifaa 4 kuimarisha Yanga msimu ujao
Uongozi wa Yanga tayari umewapokea nyota wanne wa kigeni wanaotarajiwa kusajiliwa na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema anatarajia kukamilisha usajili wa nyota sita wa kigeni pamoja na wazawa wawili kabla ya kuondoka kwenda DR Congo kujiunga na kambi ya timu ya Taifa
Nyota wa kigeni waliohudhuria mazoezi ya Yanga jana ni pamoja na kiungo mwenye umri wa miaka 20 raia wa Nigeria Victor Patrick Akpan aliyekuwa akikipiga na JKU ya Zanzibar
Akpan yuko kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Nigeria umri chini ya miaka 23
Wengine ni beki wa kati Mohammed Ali Camara mwenye umri wa miaka 21 kutoka klabu ya Horoya AC ya Guinea
Camara aliitumikia timu ya Taifa ya Guinea U20 na tayari ameitumikia timu ya wakubwa mara moja
Wengine ni mshambuliaji Shehu Magaji Bulama raia wa Nigeria na kiungo Allex Komenan kutoka nchini Ivory Coast
Bulama na Komenan watafanyiwa majaribio na Zahera kabla kuidhinisha kama wasajiliwe au la .



Comments
Post a Comment