Wachezaji United kupunguziwa mishahara
Wachezaji wa Klabu ya Manchester United watapunguziwa asilimia 25 ya Mishahara yao sababu ya kushindwa kuiwezesha Klabu kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya... Wikendi iliyopita United ililazimishwa Sare ya 1-1 dhidi ya Huddersfield na ndoto ya kumaliza Nne bora ikapotea na kuziacha Tottenham na Chelsea zikiungana na Liverpool na Man City kucheza Champions league.
Kwa mujibu wa Sky Sports, wachezaji wengi wanyr kifungu cha Pesa za makubaliano ya mauzo katika mikataba yao, watakatwa asilimia 25 ya mshahara wao baada ya klabu kushindwa kumaliza katika nafasi nne za juu katika Msimamo wa Premier league.
Paul Pogba anaepokea £300,00 kwa wiki, anatajwa ndio atakatwa kubwa zaidi kuliko wenzie, atapunguziwa £1.8m. Alexis Sanchez ambaye anatajwa kuwa nj usajili mbovu kufanywa na United yeye analipwa £500k kwa wiki Baada ya makato inabakia £375k ikiwa atasalia ndani ya Klabu hiyo kuanzia msimu ujao.
Nyota wengine ambao panga La makato litawakumba ni Mshambuliaji Romelu Lukaku anaepokea £250k nae itapungua na kufikia £187k, Mlinda lango anaetupiwa lawama Kila Mchezo anaocheza, David De Gea anaepokea £200k nae itashuka na kufikia £150k.. Kiungo wa Kimataifa wa Brazil, Fred ambaye analipwa £175k Baada ya kukatwa itafikia £131k.
Imeripotiwa kuwa, United kukosekana UCL inaweza kupoteza mpaka £65m katika Mapato ya TV, Mdhamini wao wa Jezi kampuni ya Addidas itapunguza dau lao kwa Asilimia 30 Baada ya Klabu hiyo kushindwa kufuzu Champions league, yaani zitapunguzwa £20m kati ya £750m katika dili hilo na Wadhamini wao..



Comments
Post a Comment