Salamba: nimejifunza kupitia Samatta

Namuuliza Adam Salamba...

"unajifunza nini kuhusu Samatta...?"

inaandikwa na @yasriibrahy

Soka ni mchezo wenye mambo mengi sana na mambo hayo ndio humjenga mchezaji, sio kila anaepiga mpira ni mchezaji hapana wengine tunaupiga ilii kuusogeza kwa walengwa.
Hivi ni nani ambaye alikuwaa anaimbiwa wimbo wa "samaa samaa Sama goal" pale mjini Lubumbashi na je Leo nani anaimbiwa tena wimbo huo huo tena kule Belgium...? Jibu ni Mbwana Ally Samatta.

Hivi Samatta baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika ligi ya Europa alishindwa kuwaambia GENK sitaki kuongeza mkataba akatimkia zake Uingereza hata ligi daraja la kwanza.....?
Leo tunamuona Samatta UEFA akiwa na GENK je angeondoka na kwenda Uingereza tungemsema Mtanzania gani leo kwenye UEFA.



Adam Salamba unajifunza nini kwa Samatta.....

Msimu wa ligi wa 2015/2016 na 2016/2017 ulikuwa ni msimu mzuri sana kwa Adam Salamba.
Hivi unamkumbuka Salamba wa lipuli au unamkumbuka Salamba wa Stand United. Salamba ambaye anatoka na mpira katikati ya uwanja anapiga one two na Shabani Ada anaweka mpira kwenye nyavu Simba anakufa goli 1 Iringa.
Hivi unamkumbuka Adam Salamba ambaye aliyekuwaa anafunga kila mechi katika zile mechi kumi za mwisho wa ligi akiwa Lipuli.

Hivi Salamba bado hukuzijua tuu klabu zetu kubwa mpaka ukaamua kwenda Simba, Simba ambayo kuna watu kama Okwi, Kagere, Bocco, Niyonzima.
Aah Lipuli yako inacheza Fainali ya ASFC huenda na wewe ungekuwa ni mmoja wa mashuja wa kuwafikisha Lipuli fainali kama alivyofanya kaka yako Paul Nonga, huenda pia wewe ndo ungekuwa shujaa pekee wa kuifanya Lipuli kuwa bingwa na kucheza kimataifa ukiwa wewe ndie muongozaji wa safu ya ushambuliaji.

Mfano wa maneno yangu anao Samatta ambaye alikataa kwenda Uingereza na kubaki na GENK leo tunatarajia kumuona akiongoza safu ya ushambuliaji ya GENK hiyo hiyo katika ligi ya Mabingwa Ulaya ( UEFA CHAMPIONS LEAGUE )

Muda bado upo sana Salamba....

powered by @sokakijiweni_
                      sokakijiweni.blogspot.com
                       Maisha ya SOKA tz

written by @yasriibrahy

Comments

Popular Posts