Ramos: Siondoki Madrid

-h Nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos ametangaza kuwa anatarajia kusalia na klabu hiyo mpaka msimu ujao, licha ya kupokea ofa kubwa kutoka vilabu vya Ligi ya China; Beki huyo mwenye umri wa miaka 33 alikuwa akihusishwa kuondoka klabuni hapo Baada ya kudumu miaka takribani 14.
.
- Katika mkutano na Waandishi Ramos Amethibitisha kuwa haondoki Santiago Bernabeu na kuthibitisha kupokea ofa kubwa..
-- "Mimi ni Madridista. Nataka kustaafu hapa," Ramos aliwaambia waandishi wa habari. -- "Sitaki mashabiki wabaki katika shaka yoyote, Kumekuwa na uvumi mno juu ya hatma yangu na nataka kutoa ahadi yangu kuwa nitastaafu nikiwa na hii klabu." Aliongeza mhispania huyo.
.
- Alipoulizwa kuhusu uhusuano wake na rais wa klabu Florentino Perez, aliongeza: "Uhusiano wangu na rais ni sawa na wa baba na mwana."
.
- Alipouluzwa kuhusu kupokea ofa kutoka vilabu vya China, Ramos Alithibitisha kuwa ni kweli Kuna ofa kutoka China, Lakini sasa mpango wake ni kuwa na Real Madrid mpaka ataksposema yeye na Soka inatosha..

Comments

Popular Posts