Polisi Tanzania wapanda ligi kuu Tanzania Bara kwa kishindo....

POLISI TANZANIA YAPANDA DARAJA

Timu ya Polisi Tanzania imefanikiwa kupanda daraja kucheza Ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Boma FC katika mechi za mwisho za ligi hiyo zilizopigwa leo.

Matokeo hayo yameifanya Polisi waliokuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Ushirika Mjini Moshi kufikisha pointi 47 na kuongoza kundi A hivyo kuungana na Namungo FC ya Lindi ambao ni vinara wa Kundi B  kupanda daraja moja kwa moja.

Timu nyingine mbili zitapatikana baada ya kuchezwa kwa mechi za mtoano (Play Off) zikihusisha timu mbili zilizoshika nafasi ya pili na ya tatu kutoka kila kundi pamoja na timu mbili zitakazomaliza ligi kuu zikiwa kwenye nafasi ya 17 na 18.

Kwa kuangalia msimamo wa makundi yote mawili timu zitakazocheza play off kusaka nafasi ya kupanda daraja kutoka Kundi A ni Pamba SC na Geita Gold na kutoka Kundi B ni Mbeya Kwanza na Mlale JKT.


Comments

Popular Posts