Namuona Samatta kule alipo Ronaldo, Messi, Hazard na Neymar
Namuona Samatta
Kwa mara ya kwanza toka dunia imeumbwa haijawahi tokea mtanzania Kucheza Europa ila Mbwana Ally Samatta pekee ndiye aliye peperusha bendera ya Tanzania katika michuano hiyo.
Kwa mara ya pili toka dunia imeumbwa haijawahi tokea mtanzania kucheza UEFA ila Mbwana Ally Samatta pekee ndiye anaye enda kuipeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya ligi ya mabigwa barani Ulaya UEFA.
Waswahili husema " lisemwalo lipo kama halipo basi linakuja"
Namuona Samatta katika timu kubwa barani ulaya kwa siku za usoni, Kiwango alichoonesha nahodha huyo WA timu ya Taifa ya Tanzania ni kiwango cha hali ya juu ambacho kinashawishi kila timu kubwa barani Ulaya kuweza kunyemelea saini ya Mbwana Ally Samatta.
#HainaKuferi hii ndio kauli mbiu ya Mbwana Ally Samatta na matunda ya kauli hii nadhani leo kila mtu anaiona bila kuhadisiwa.
#NIDHAMU na #KUJITUMA ndio silaha yangu alisema Samatta kipindi yupo TP MAZEMBE.
Kila la kheri Nahodha Mbwana Ally Samatta
powered by @yasriibrahy
@sokakijiweni_
Maisha ya SOKA tz



Comments
Post a Comment