Mazembe waongeza dau kwa Ajibu

JE UNAJUA DAU LA IBRAHIM AJIBU KWA KLABU YA TP MAZEMBE YA NCHINI CONGO?

 Straika wa Yanga,Ibrahim Ajibu  fundi wa mpira, anayetakiwa na TP Mazembe, imebainika anataka kujiunga na miamba hiyo ya Congo huku akiwa na mkataba wa awali wa Simba.

Ajibu, anayeongoza kwa kuasisti katika ligi ya msimu huu akitoa pasi 15 za mabao huku mwenyewe akifunga sita, yupo mbioni kujiunga na Mazembe ambayo imetuma barua Yanga ili kumbeba mara baada ya mkabata wake kumalizika Juni 30 mwaka huu.

Mazembe imewaandikia barua Yanga kuwajulisha kuwa watamchukua Ajibu rasmi Julai mosi 2019 na kwamba kama kuna utofauti wowote wa taarifa hiyo Yanga iwasiliane nao kwa mujibu wa Kanuni za Usajili za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).


Habari za kuaminika kutoka Yanga zinasema, Mazembe wapo tayari kumbeba Ajibu kwa kitita cha zaidi ya Dola 25,000 (karibu Sh 60 Milioni), mbali na mshahara mnono na huduma nyingine zikiwamo usafiri, makazi na posho nyingine za kutosha.


Chanzo hicho kilidokeza mkataba wa nyota huyo umetazamwa katika vipengele muhimu ikiwa sambamba na fedha ya mshahara na nafasi ya kumruhusu kutoka endapo atapata timu nyingine ya kucheza.

  Katika dili hilo Yanga ni wazi haitapata fedha zozote kwani usajili huo umekuja Ajibu akiwa amemaliza mkataba, huku ikielezwa Simba walishamsainisha mkataba wa awali wa kumsajili kabla ya Moise Katumbi na watendaji wake kutaka kupindua meza.

Comments

Popular Posts