Madrid kutoa £52.4m (€60m) kumnasa Luka Jovic wa Frankfurt ya Ujerumani

✍🏼 Sasa ni suala la muda tu, Luka Jovic amekamilisha uhamisho wa £52.4m (€60m) kujiunga na Real Madrid ya Hispania akitokea Eintracht Frankfurt ya Ujerumani.
:
✍🏼 Nyota huyo wa Kimataifa wa Serbia mwenye umri wa miaka 21, amekubali Mkataba wa miaka Mitano kuwatumikia miamba hao wa Hispania, ambapo ataingiza £43.7m na kwa mwaka itakuwa ni £8.7m Kipindi chote; Klabu yake ya Sasa, Frankfurt itailipa Klabu ya zamani ya nyota huyo Benfica ya Ureno £10.5m Kama makubaliano yao walivyopeana Mchezaji huyo.


:
✍🏻 Jovic alijiunga na Frankfurt kwa mkopo kutoka Benfica mwanzoni mwa msimu, lakini katika mwezi uliopita Klabu hiyo ya Bundesliga iliweka kipengele cha kumnunua, tangu alipojiunga nao Jovic amefunga mabao 17 katika mechi 31 za Bundesliga msimu huu na magoli 10 katika Europa League, ambapo Frankfurt ilipoteza mbele ya Chelsea kwa Penati katika nusu fainali..
#laliga #bundesliga #realmadrid

Comments

Popular Posts