Ajibu akataa kwenda TP Mazembe, atimkia Simba



NASIKITIKA KUONA/KUSIKIA IBRAHIM AJIBU HATAKI KWENDA TP MAZEMBE

Najiuliza hivi sisi watanzania tuna mawazo gani? Hadi tunashindwa kuona fursa za wazi kama hizi? Sijui malengo yake kusema la ukweli. Barua inaeleza hawajakubaliana maisha binafsi.. Baadhi ya taarifa zinasema tayari alikwisha saini klabu ya Simba SC🇹🇿. Najiuliza kweli, hawa wachezaji wana malengo gani?

Huenda TP Mazembe🇨🇩 walitaka kumpa dau dogo la usajili kuliko alilopewa Simba SC🇹🇿.. Inawezekana. Ila kitu kimoja tofauti, kucheza TP Mazembe🇨🇩 kunakupa fursa nzuri zaidi ya kupiga hatua ya soka kuliko kucheza Simba SC🇹🇿. Kwann nasema hivi, ukiangalia rekodi za usajili za klabu hizo ni tofauti, kiufupi Mazembe ni kioo zaidi kwa mchezaji kuliko Simba SC🇹🇿.


Faida ambayo huenda angeipata Ajibu pale TP Mazembe🇨🇩 ni kukutana na wachezaji wenye malengo makubwa na wanaojielewa, kucheza michuano yenye ushindani mkubwa na kufika hatua nzuri, kucheza ligi yenye ubora na ushindani. Kukaa kwake na kina Trésor Mputu, Christian Koffi, Sylvan Gbouhou, Issama Mpeko, Jackson Muleka, Meshack Elia, Chongo na wengine kungemjenga zaidi kimalengo. Siku zote naamini unapokaa na kundi la watu wanaojitambua na ww ni rahisi kujitambua.

Kucheza kwake TP Mazembe🇨🇩 pia kungelinufaisha taifa. Sidhani kama angeshuka kiwango TP Mazembe🇨🇩. Kulingana na ushindani wa namba, na aina ya wachezaji... Lazima angepandisha kiwango na kuwa na uzoefu mkubwa wa kiprofeshno..

Huenda bado vijana wetu hawana malengo ya mbali, waliyonayo wachache tayari wapo zao wanafaidika na viwango vyao. Mtu kama Ibrahim Ajibu inasikitisha sana kuona anaishia kucheza soka hapa hapa Tanzania. Kipaji alichonacho, kama akiongeza jitihada zaidi... Naamini pale TP Mazembe🇨🇩 angeweza kurithi mikoba ya Trésor Mputu, ambaye umri unamtupa mkono.

Kwa hili, Ajibu na washauri wake wamekosea. Kwenda kwake TP Mazembe🇨🇩 kungehisabika kupiga hatua kuliko kurudi Simba SC🇨🇩.


Comments

Popular Posts