RC MAKONDA ATOA SHEHENA YA FUTARI DAR ES SALAAM



.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. @baba_keagan ametoa *shehena ya Futari* ikiwemo *Sukari, Mchele, Unga, Maharage na Mafuta* kwa zaidi ya *Watu 350 kutoka Makundi* mbalimbali ikiwemo *Yatima, Walemavu wa Viungo, Wasioona,* Watu wenye *ulemavu wa Ngozi Albino* na Watu *wasiojiweza* kama sehemu ya *sadaka ya Mwezi mtukufu wa Ramadhan.*

Katika Shehena hiyo aliyotoa *RC Makonda* kila Mwananchi amepata vifurushi vyenye *Mchele Kilo 5, Unga kilo 5, Sukari, kiroba cha Maharage na Mafuta ya kupikia*.

Msaada huo wa Futari aliotoa *RC Makonda* umetoka kwenye Taasisi ya *MIRAAJ TANZANIA* iliyompatia Vitu hivyo kama sehemu ya kuunga mkono juhudi zake na *RC Makonda* akaelekeza vitu hivyo vitolewe kwa *watu wa wasiojiweza* katika jamii ili Waweze kupata ahueni Kipindi hiki cha Mfungo.

Akitoa Futari hiyo kwa walengwa kwa niaba ya *RC Makonda*, Mkurugenzi wa Taasisi ya Miraaj Tanzania *Bw. Arif Tanzania* amesema Taasisi hiyo imekuwa na *imani kubwa* na Mkuu wa Mkoa kwakuwa *kila msaada anaopatiwa anaufikisha kwa walengwa* tena kwa *uwazi Mkubwa*.

Aidha *Bwana Arif* amesema Taasisi hiyo itaendelea kumuunga mkono *RC Makonda* katika kila jambo kwakuwa amekuwa kiongozi *anaegusa maisha ya Watu wa Makundi mbalimbali ndani ya Jamii*.

#MakiniUpdate

Comments