Mrisho Gambo: Miradi yote ya fedha ikamilike kabla ya kuanza Mwaka mpya wa fedha.
#MakiniUpdate
#ARUSHA :- *MKUU wa wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro, amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dkt. Maulid Madeni kuhakikisha miradi yote ya Maendeleo ya mwaka wa fedha 2019-20 inakamilika kabla ya kuanza kwa mwaka mpya wa fedha.*
Daqarro ametoa agizo hilo leo Aprili 21 mwaka huu wakati akikagua jengo la utawala la shule ya sekondari ya Terati ambalo halijakamilika.
Akitoa ufafanuzi wa kutekeleza maagizo hayo mkurengenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ya Jiji la Arusha Dk. Madeni, amesema amesimamisha fedha zote za matumizi ya kawaida kwa ajili ya kuwalipa wakandarasi wanaoendelea na ujenzi maeneo mbalimbali ya miradi ya Maendeleo.
Dkt. Madeni amesema hadi kufikia Mei 30 miradi yote ya mwaka wa fedha wa 2019-20 ambayo iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji itakuwa imeshakamilika kwa ajili ya kuanza kututoa huduma.

Comments
Post a Comment