Majaliwa, wanasiasa msitumie mlipuko wa virusi vya corona kujipatia umaarufu

#Habari

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaasa wanasiasa nchini kutotumia mlipuko wa virusi vya corona unaoendelea kuua Watu China, kujipatia umaarufu wa kisiasa 'tusipotoshe Umma'

Waziri Mkuu amesema hayo kwenye Msikiti wa Gaddafi Dodoma ambapo amesisitiza pia umuhimu wa Watanzania kuliombea Taifa ili Mungu aliepushe na maafa.

"Mji wa Wuhan ambako virusi vilianzia wapo Vijana 497 wa Kitanzania na wote wapo salama, na bado Serikali inaendelea kuwasiliana nao"


Comments