Leno aondolewa timu ya taifa (Ujerumani)
- Mlinda lango, Bernd Leno ameondolewa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kwa michezo ijayo ya kuwania kufuzu kwa EURO 2020 dhidi ya Belarus na Estonia kutokana na kuumia, nafasi yake imechukuliwa na Sven Ulreich.
.
- Leno, mwenye umri wa miaka 27, alikuwa kwenye benchi Klabu yake ya Arsenal wakati ikipokea kipigo cha Magoli 4-1 dhidi ya Chelsea katika fainali ya Europa League siku ya Jumatano, lakini amekuwa akiripotiwa kuwa mgonjwa kwa wiki kadhaa hivi Sasa.
.
- Hajawahi kuichezea Ujerumani tangu Disemba 2017, na nahodha Manuel Neuer bado anachaguliwa kuwa chaguo la kwanza na Marc-Andre ter Stegen na Kevin Trapp wakipigania nafasi ya Pili kwenye benchi.
.
- Mlinda lango wa Barcelona Ter Stegen nae hajaitwa Sababu ya kuwa Majeruhi, Leno aliitwa pamoja na makipa wengine Neuer na Trapp kwa ajili ya michezo hiyo ya Juni 8 na Juni 11, lakini kuondolewa kwake maana yake ni kwamba Kipa wa Bayern Munich, Sven Ulreich amepewa nafasi katika kikosi ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya Soka..

Comments
Post a Comment