Kapombe akanusha wanaomzushia kaumia tena
"Ni jambo la kusikitisha na linaloumiza kwa kiasi kikubwa kwa taarifa hii inayoendelea kusambazwa na vyombo vya habari na watu mbalimbali kuwa nimeumia /nimejitonesha jeraha langu hakika hizi habari sio za kweli kabisa na hazina uhakika na ukweli wowote, katika siku niliyoumia ni leo najiuliza nitaumiaje nikiwa nipo nyumbani na kambini sijaingia au kufanya mazoezi na timu ya Taifa???
Mimi niko mzima na nafanya mazoezi yangu vizuri nafuata programu yangu niliyoachiwa na Mwalimu wa Viungo wa Simba.
Mimi pamoja na familia yangu tumeumizwa na taarifa hii ni kubwa na nzito kwetu naomba vyombo vya habari kutoa taarifa iliyokuwa sahihi na yenye ukweli wa 100%.
Wanasimba na Watanzania wote, wapenda soka napenda kuwaambia kuwa mimi niko sawa na hakuna ukweli wowote kuhusu mimi kuumia tena hizi taarifa sio sahihi kwa wote waliyotoa taarifa hizi au kusambaza.... Mungu nipe uvumilivu na haya yatapitaπππππ"- Shomari Kapombe akikanusha taarifa ambazo zinasambaa kwamba ameumia tena.

Comments
Post a Comment